LIMA:Idadi ya watu waliouwawa kwenye tetemeko la ardhi yaongezeka
16 Agosti 2007Matangazo
Idadi ya watu waliouwawa kufuatia tetemeko la ardhi lenye kasi ya vipimo vya rishta 7.9 imeongezeka na kufikia watu 337 nchini Peru.
Takriban watu wengine 1000 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo lililokumba umbali wa kilomita 148 kusini mwa mji wa Lima.
Serikali ya Peru imetangaza hali ya hatari huku tetemeko hilo likisambaza hali ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa mji mkuu wa Lima.
Watu wamelazimika kuondoka kwenye majumba kuepuka maafa.