Lekerkusen yatamba katika michuano ya Ulaya | Michezo | DW | 18.02.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Lekerkusen yatamba katika michuano ya Ulaya

Bayer Levekusen imetamba ugenini katika michuano ya kombe la Ulaya kwa kuikandika Metalist Kharkiv ya Ukraine mabao 4-0

default

Wachezaji wa Leverkusen Renato Augusto, Michal Kadlec na Hanno Balitsch wakishangilia moja kati ya mabao 4 waliyofunga dhidi ya FC Metalist Kharkiv

Yalikuwa ni mabao ya Eren Derdiyok,Gonzalo Castro na Sidney Sam aliyepachika mawili, yaliyoipatia ushindi mzito Leverkusen na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Katika mechi nyingine za michuano hiyo ya kombe la Ulaya, timu nyingine ya Ujerumani, Stuttgart, ilichapwa mabao 2-1 na Benfica ya Ureno mjini Benfica.

Stuttgart ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Martin Harnik, kabla ya Benfica kusawazisha na kuongeza la pili. Hata hivyo, bao hilo la ugenini linaiweka katika nafasi nzuri Stuttgart ya kusonga mbele.

Ama Liverpool ilitoka suluhu bin suluhu na Sparta Prague mjini Prague, matokeo kama hayo pia yakijitokeza katika mechi kati ya Napoli ya Italia na Villarreal.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Othman Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com