1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Maonyesho ya Vitabu ya Frankfurt

Maonyesho ya Vitabu ya Frankfurt (Frankfurter Buchmesse) ndiyo maonyesho makubwa zaidi ya vitabu duniani kwa muktadha wa idadi ya makampuni ya uchapishaji yanayowakilishwa, na idadi ya wageni.

Maonyesho ya vitabu ya Frankfurt yanachukuliwa kuwa maonyesho muhimu zaidi ya vitabu duniani kwa ajili ya miamala na biashara ya kimataifa. Tukio hilo la siku tano katikati mwa Oktoba linafanyika katika viwanja vya maonyesho ya biashara vya Frankfurt, mjini Frankfurt am Main, nchini Ujerumani. Maelfu ya waonyeshaji wa kimataifa, wakiwakilisha makampuni ya uchapishaji wa vitabu, vyombo tofauti vya habari na teknolojia, na vilevile waotoaji wa maudhui kutoka duniani kote, hukusanyika pamoja ili kujadiliana juu ya haki za uchapishaji na ada za leseni. Maonyesho hayo huandaliwa na Frankfurter Buchmesse GmbH, kampuni tanzu ya chama cha wachapishaji na wauzaji vitabu cha Ujerumani. Zaidi ya waonyeshaji 7,300 kutoka zaidi ya mataifa 100, na karibu wageni 300,000 hushiriki maonyesho hayo.