Lagos:Mhandisi wa mafuta wa Kimarekani aachiwa huru katika eneo la Niger Delta, Nigeria | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Lagos:Mhandisi wa mafuta wa Kimarekani aachiwa huru katika eneo la Niger Delta, Nigeria

Watekaji nyara katika eneo linalotoa mafuta la Niger Delta huko Nigeria wamemuachia huru mhandisi wa Kimarekani na dereva wake wa kutokea Nigeria. Wote wawili walishikiliwa tangu Januari 20. Watu waliokuwa na bunduki waliwakamata mahabusu hao walipojuwa wakienda kazini katika mji mkubwa wa Port Harcourt. Kuachiliwa watu hao kunawabakisha raia sita wa kigeni bado katika mikono ya watekaji nyara ambao ni makundi ya wahalifu. Maelfu ya ya wafanya kazi wa kigeni wa visima vya mafuta wamelihama eneo hilo la Niger Delta mnamo mwaka uliopita kwa vile mashambulio na utekaji nyara yamekuwa ni mambo yanayotendeka kila wiki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com