Kesi dhidi ya raia wa Ufaransa kwa kudaiwa kuwateka nyara watoto 103 yaanza nchini Tchad | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Kesi dhidi ya raia wa Ufaransa kwa kudaiwa kuwateka nyara watoto 103 yaanza nchini Tchad

NDJAMENA:

Raia 6 wa kifaransa wanaofanya kazi za utoaji misada na kushtumiwa kuwateka nyara watoto 103 wanasimama kizimbani Ijumaa.Watu hao ni watumishi wa shirika la kiutu linaloitwa Zoe’s Ark na walikamatwa mwisho wa mwezi wa Oktoba wakijaribu kuwasafirisha watoto hao kutoka Tchad hadi Ulaya. Washukiwa wanadai kuwa walikuwa wanawahamisha mayatima wa Darfur kwa famila za Ulaya,ingawa uchunguzi unaonyesha kuwa hakuna kati ya watoto hao aliekuwa yatima wala kutoka mkoa wa matatizo wa Darfur nchini Sudan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com