KABUL: Waafghanistan wanane wauwawa katika shambulio la majeshi ya NATO | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Waafghanistan wanane wauwawa katika shambulio la majeshi ya NATO

Shambulio la angani la jeshi la NATO limewaua raia takriban wanane wa Afghanistan katika mkoa wa Kandahar kusini mwa nchi hiyo. Raia wengine tisa wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Gavana wa mkoa wa Kandahar, Asadullah Khalid, amesema vifo hivyo vimesababishwa na mabomu ya NATO yaliyoyapiga makaazi matatu katika wilaya ya Zhari mkoani humo.

Shirika la NATO limesema linajutia vifo vya raia hao na linafanya kila juhudi kupunguza uwezekano wa kutokea maafa wakati wa operesheni zake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com