Juhudi za uokozi zakwama Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.08.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Juhudi za uokozi zakwama Pakistan

Mvua nying za masika zinaendelea kuzikwamisha harakati za uokozi katika maeneo mengi yaliyoathiriwa na mafuriko nchini Pakistan.

Maji yaliyotuama Kot Addu,Punjab- Pakistan

Maji yaliyotuama Kot Addu,Punjab- Pakistan

Mafuriko hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 80 ,yamesababisha vifo vya kiasi ya zaidi ya watu 1600 na wengine milioni 12 wameachwa bila makazi.

Ndege za uokozi zililazimika kuzikatiza safari za kuelekea kwenye maeneo yaliyoathiriwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa na kina kinachoongezeka cha maji ya mito iliyofurika iliyoyasomba madaraja.Hali hiyo imeshuhudiwa katika maeneo ya kaskazini magharibi ya Khyber-Pakhtunkwa ambako harakati za uokozi zimekwama hususan katika maeneo ya vijijini. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na janga hilo Jean–Maurice Ripert ameusisitizia umuhimu wa msaada wa jamii ya kimataifa

Pakistan Flut Katastrophe 2010 Flash-Galerie

Waathiriwa wa mafuriko wakiminyana kupata chakula cha msaada.

Mjumbe huyo aliizuru Pakistan ili kujionea hali halisi itakayomuwezesha kufanya tathmini kamili ya msaada unaohitajika.Kulingana na watabiri wa hali ya hewa,mito miengine 10 huenda ikafurika na mvua nyingi zaidi inatarajiwa kunyesha katika kipindi cha saa 48 zijazo katika eneo la kaskazini.Kwa upande wake Waziri Mkuu Yousef Raza Gilani amekiri kuwa nchi yake haina uwezo wa kukabiliana na janga hilo na ameitolea jamii ya kimataifa wito wa kuipa msaada wa dharura wa aina yoyote.Serikali ya Pakistan imenyoshewa kidole na wakazi wake walioathirika ambao bado hawajapata msaada wowote.

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com