Mafuriko yaua zaidi ya watu 800 nchini Pakistan. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mafuriko yaua zaidi ya watu 800 nchini Pakistan.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema mvua za masika zitaendelea kunyesha kwa siku 10 zijazo.

Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni 1 wamepoteza makaazi yao nchini Pakistan.

Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni 1 wamepoteza makaazi yao nchini Pakistan.

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 80 kaskazini magharibi mwa Pakistan, imeongezeka hadi 830. Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko hayo. Takriban madaraja 45 yameharibiwa katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa pekee. Madaraja hayo pamoja barabara zilizojaa maji yanavuruga jitihada za waokoaji katika jaribio lao la kuwafikia wahanga. Mito iliyofurika kutokana na mvua za msimu wa masika imefunika vijiji na kusomba miundo mbinu ya mawasiliano.

Überschwemmung in Pakistan

Mafuriko hayo ni mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 80 nchini Pakistan.

Umoja wa Mataifa umeahidi kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahanga. Serikali ya Ujerumani imetoa Euro nusu milioni kama msaada wa dharura. Marekani inatuma helikopta kadhaa zisaidie katika juhudi za uokozi.

Mwandishi, Peter Moss/Reuters/AFP

Mhariri, Mohamed Dahman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com