1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za uokoaji wa maafa ya maporomoko nchini Uganda zaendelea

3 Machi 2010

Juhudi za kutafuta watu waliyonusurika kufuatia maporomoko ya matope katika mlima Elgon, zinaendelea.

https://p.dw.com/p/MIiz
Waokoaji katika kijiji cha Bududa , Mashariki mwa Uganda wakiendelea kuwatafuta wahangaPicha: picture-alliance/Photoshot

Hata hivyo, kutokana na ugumu wa eneo yalikotokea maafa hayo, magari na vifaa vikubwa vya uokozi hayawezi kufika, hivyo waokozi wamekuwa wakitumia mikono kufukua watu waliofunikwa na matope hayo. Inakadiri kuwa zaidi ya watu mia tatu wamefunikiwa , huku maiti kiasi ya 80 mpaka sasa ndizo zilizopatikana.

Mwandishi wa Kampala Leyla Ndinda amekwenda katika eneo hilo la maafa, na Aboubakary Liongo amezungumza naye muda mfupi tu uliyopita akiwa anapanda mlima kuelekea katika vijiji vilivyofikwa na maafa hayo.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Othman Miraji