JERUSALEM.Polisi watumia gesi ya machozi na risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji | Habari za Ulimwengu | DW | 09.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM.Polisi watumia gesi ya machozi na risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji

Polisi wamelazimika kuingia katika maeneo ya msikiti wa Al Aqsa mjini Jerusalem ili kuwatawanya wapalestina waliokuwa wanafanya vurugu.

Polisi hao iliwabidi kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za plastiki dhidi ya wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.

Maandamano hayo yalianza kutokana na uchimbaji unaoendelea karibu na eneo la kale la Temple Mount ambalo ni eneo takatifu kwa waislamu linalojulikana kama Haram al Sharif.

Wapalestina wanapinga uchimbaji huo, wanahofia kuwa utaharibu msingi wa eneo hilo takatifu.

Utawala wa Israel umesisitiza kuwa kazi hiyo itaendelea na kutoa hakikisho kuwa hakuna uharibifu wowote utakaotokea katika eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com