JAKARTA: Watu takriban 60 wauwawa kwenye tetemeko la ardhi | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Watu takriban 60 wauwawa kwenye tetemeko la ardhi

Watu wasiopungua 60 wameuwawa leo kufuatia tetemeko la ardhi kwenye kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia. Mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye tetemeko hilo la kipimo cha 6.3 kwenye vipimo vya Richter.

Tetemeko hilo limeyatikisa meneo ya nchini Malaysia na Singapore ambako watu wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao.

Katika mji wa Padang, mji mkuu wa jimbo la Sumatra Magharibi, tetemeko hilo limezusha hofu miongoni mwa wakaazi wakifikiri huenda likazusha tsunami.

Duru za polisi zinasema majengo mengi yameporomoka na idadi ya vifo huenda ikaendelea kuongezeka kwa sababu juhudi za uokozi hazijashika kasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com