Jakarta. Aceh yakamilisha uchaguzi wa serikali za mitaa. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jakarta. Aceh yakamilisha uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kundi la kimataifa la wachunguzi wa uchaguzi lililoongozwa na umoja wa Ulaya limemaliza ujumbe wake katika jimbo la Indonesia la Aceh. Kundi hilo lilikuwa katika jimbo hilo kwa zaidi ya mwaka kuangalia makubaliano ya amani kati ya serikali na waasi wa Free Aceh Movement makubaliano ambayo yamemaliza miongo kadha ya machafuko. Kazi ya ujumbe huo wa kimataifa ilikuwa ni kuangalia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mapema wiki hii. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameueleza ujumbe huo kuwa wa mafanikio.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com