ISLAMABAD : Serikali yatupilia mbali wito wa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Serikali yatupilia mbali wito wa Marekani

Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imetupilia mbali wito mpya wa Marekani wa kurudishwa kwa utawala wa katiba na kuwa na uchaguzi huru na wa haki kuwa hauna jipya.

Taarifa ya wizara hiyo imekuja baada ya Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Negraponte kukutana na Rais Pervez Musharraf mjini Islamabad kwa mazungumzo yaliolenga juu ya utawala wa hali ya hatari uliowekwa nchini humo mapema mwezi huu na uchaguzi unaokuja.

Negraponte amesema ameihimiza serikali ya Pakistan kuachana na hatua hizo,kuondowa utawala wa hali ya hatari na kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na kwamba utawala wa hali ya hatari hauendi na uchaguzi huru wa haki na wa kuaminika ambao unahitaji ushiriki wa kitendaji wa vyama vya kisiasa,vya kijamii na vyombo vya habari.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani amekwenda Pakistan hapo Jumamosi na alizungumza kwa simu na waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto ambaye serikali ya Marekani inataka aanze tena mazungumzo ya kushirikiana madaraka na Musharraf lakini Bhutto amefuta uwezekano wa mazungumzo hayo na kuapa kwamba katu hatotumika bega kwa bega na Musharraf.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com