ISLAMABAD : Rais Musharraf kun’gatuka ukuu wa majeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Rais Musharraf kun’gatuka ukuu wa majeshi

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amesema kwamba atajiuzulu wadhifa wa mkuu wa majeshi kabla ya tarehe Mosi Desemba.

Tangazo hilo linakuja wakati mtawala huyo wa kijeshi alieingia madaraka kwa mapiduzi yasio na umwagaji damu hapo mwaka 1999 na hivi karibuni kutangaza utawala wa hali ya hatari akikabiliwa na ongezeko la shinikizo la kimataifa linalomtaka aachane na wadhifa huo wa kijeshi.

Musharraf huko nyuma alisema atasubiri Mahkama Kuu ipitishe hukumu juu ya uhalali wa kuchaguliwa tena kuwa rais katika uchaguzi wa Oktoba tarehe sita kabla ya kun’gatuka jeshini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com