1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yakosoa mipango ya kurekebisha uhusiano na Israel

1 Mei 2024

Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei, amesema juhudi za kurekebisha mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu, hazitatatua mzozo wa Mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/4fOwx
Iran yakosoa mipango ya kurekebisha uhusiano kati ya mataifa yakiarabu na Israel
Iran yakosoa mipango ya kurekebisha uhusiano kati ya mataifa yakiarabu na IsraelPicha: Iranian Supreme Leader's Office/ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Matamshi ya Khamenei yamekuja wakati waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken aliposema nchi yake inakaribia kuwa tayari na mpango wa usalama kwa Saudi Arabia  iwapo itarekebisha mahusiano yake na Israel.

Taifa hilo la kiarabu limekuwa katika mazungumzo ya kurekebisha mahusiano hayo, lakini yakasimamishwa kwa muda wakati vita kati ya Israel na Hamas vilipoanza. Wasiwasi wa kikanda umeongezeka tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyoingiliwa pia na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Syria, Lebanon, Iraq na Yemen.

Iran inaliunga mkono kundi la Hamas lakini imekanusha kuhusika moja kwa moja na shambulizi la kundi hilo kusini mwa Israel.