IPSWICH: Mshukiwa wa mauaji ya mahakaba afikishwa mahakamani | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

IPSWICH: Mshukiwa wa mauaji ya mahakaba afikishwa mahakamani

Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 amefikishwa mahakamani kwa mauaji ya makahaba watano katika mji wa pwani wa Ipswich nchini Uingereza.

Hapo awali muongozaji mashtaka walisema Stephen Wright alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji ya wanawake hao.

´Mwanamume wa pili Stephen Wright kutoka Ipswich ameshtakiwa kwa mauaji ya wanawake wote watano.´

Kushtakiwa kwa mwanamume huyo kunafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na pilisi. Kesi hiyo itasikilizwa tena Januari mbili mwakani.

Mwanamume wa pili aliyekuwa pia anazuiliwa wiki hii kuhusiana na mauaji hayo ameachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka yoyote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com