Hukumu mbili za Mahkama za Ujerumani: | Magazetini | DW | 10.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Hukumu mbili za Mahkama za Ujerumani:

Moja kumhusu gaidi na nyengine ruzuku kwa wasafiri ndio mada kuu.

Uchambuzi katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umetuwama juu ya mada moja-hukumu ya jana ya Mahkama Kuu ya Ujerumani juu kufutwa kwa ruzuku iliotolewa kwa walipa kodi wsanasafiri masafa marefu kwenda makazini-pendlerpauschale-kama inavyitwa.

Hata ile hukumu ya mlibanon alietaka kuripua gari la moshi Youssef El H. imechambuliwa.

Ilikua zamu ya ramadhan ali tena kuwakagulia safu hizo za wahariri na anaanza na hukumu ya Youssef: Gazeti la Dresdner Neueste Nachrichten laandika:

"Youssef El H. hakumuonya abiria yoyote kabla bomu kuweza kuripuka.Amekiri pia kitendo alichopanga ingawa baadae alikanusha aliosema.Yote hayo yanalingana kabisa na nadharia ya mtu ambae akiumia kwa kubanawa mno na matarajio ya ukoo wake maishani mwake, wakati kaka yake yumo kizuizini akishukiwa ugaidi.Ni kijana alietaka kusomea uhandisi katika nchi hii ya maadui zake na ambae mashujaa wake anaowapigia mfano mbali na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani,Michael Ballack,bali pia Osama bin Laden na Al-Sarkawi.

laiti bomu katika treni ile ya kimkoa lingeripuka,mwanafunzi huyo alieshindwa kusoma Youssef El H,angejihisi binafsi na kwa macho ya nduguye ni shujaa aliejitoa mhanga.Shujaa kama vile Ballack na Bin laden.Sasa atasononeka korokoroni akitumai atafunzwa jinsi ulimwengu hasa ulivyo..."

Gazeti la Westfalenpost likiendeleza mada hii linasema kwamba mshtakiwa huyo aliapa kwa jina la Mwenye Enzi Mungu kwamba hakuwa kabisa na azma ya kumua yeyote.Lakini ishara zote na ushahidi wote unabainisha hiyo ndio iliokua azma yake.Gazeti laongeza :

Yeye ni mmoja kati ya watu 2 ambao katika mwaka wa shangwe za kombe la dunia hapa Ujerumani,alipanga kuzimaliza shangwe hizo kwa bahari ya damu katika gari-moshi.Ghadhabu na chuki zake kwa ulimwengu wa kimagharibi,kuelemea dini ,ziliripuka baada ya kuchapishwa vile vikatuni vilivyomdhihaki Mtume Muhammad.Ujerumani kwahivyo, haikuwahi kukaribua kujionea shambulio kubwa la wafuasi wenye itikadi kali ya kiislamu kama mara hii.Kwahivyo, kupewa kifungo cha maisha kwa (Youssef) ni adhabu iliostahiki....

Likitugeuzia mada ,gazeti la Volkszeitung linaichambua hukumu nyengine ya mahkama-ile ya Mahkama kuu ya Ujerumani iliotoka jana kuhusu ruzuku kwa wasafiri wanaoishi mji mmoja kwenda kufanya kazi mji mwengine:

Serikali iliifuta ruzuku hiyo kwa wale wasiopindukia km 21. Leipziger Volkszeitung laandika:

Mahakimu wa Mahkama Kuu iliwabidi tena kuikaripia serikali.Kwa hukumu hiyo mamilioni ya wasafiri sio tu wametunukiwa sasa zawadi kabla ya X-masi,bali wanarejeshewa kile serikali ilichowapokonya.Serikali ilipoweka mpaka juu ya kanuni hii,shaka-shaka nyingi za kisheria zilichomoza ikibainika kanuni ya usawa kwa wote kikatiba imekiukwa....."

Likitukamilishia, gazeti la Sudwest Presse laonya:

"Mashabiki wa ruzuku hizo wasifanye pupa ya kushangiria mno:Serikali ina mamlaka ya kuongoza au kurahisisha sheria za kodi.Na sasa inabidi kufanya juhudi kuwaeleza wananchi busara ya hatua zake.Hifadhi ya mazingira katika wakati huu wa kuchafuka hali ya hewa ni hoja yenye nguvu kuwa ruzuku kama hizo kwa wasafiri na jinsi ya kuzitoa kuzizingatia upya ."