Hearts of Oak nje ya kombe la Afrika | Michezo | DW | 03.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hearts of Oak nje ya kombe la Afrika

Wakati mabingwa wa zamani Hearts of Oak (Ghana) wako nje ya kombe la Afrika,B.Munich imeitoa Schalke 04

Miroslav klose anasa wavu wa Schalke.

Miroslav klose anasa wavu wa Schalke.

Katika kinyan’ganyiro cha kombe la Afrika la klabu bingwa , mabingwa wa zamani Hearts of oak kutoka ghana wamepigwa kumbo hapo jana na FC 105 ya Gabon wakati simba ya Tanzania sasa ina miadi na Enyimba ya Nigeria duru ijayo.Young Africans yatamba mbele ya Adema kwa mabao 2:0 na inasonga mbele pia duru ijayo.Tutasikia mapya katika viwanja vya michezo huko Kenya baada ya utulivu kurejea.

Katika changamoto ya Bundesliga kati ya simba 2,ni Bayern Münich mwishoe ilionguruma mbele ya Schalke kwa bao 1:0.

Leverkusen ilikiona kilichomtoa kanga manyoya ilipozabwa mabao 2:0 na chipukizi Bochum.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza –mwanya wa Arsenal kileleni umezidi kupunguzwa mwishoni mwa wiki na sasa umesalia pointi 1 baada ya Arsenal kutoka sare tu bao 1-1 na Aston villa wakati mahasimu wao mabingwa Manchester United

Waliikumta Fulham kwa mabao 3-0.

Tukianza na kombe la klabu bingwa barani Afrika,mabingwa wa zamani wa kombe hilo Waghana Hearts of oak wameaga kombe na mapem baada ya kaburi waliochimbiwa Libreville wiki 2 nyuma,kuwazika jana nyumbani Accra licha ya kushinda mpambano wao wapili wa duru ya kwanza ya kombe hili.Ushindi wa Hearts of Oak jana wa mabao 3-1 nyumbani haukutosha kuwazuwia wanajeshi wa Gabon –FC 105 kutoroka na tiketi ya kucheza duru ya pili ya champions League.

Kuaga mashindano kwa Hearts of Oak kulitanguliwa siku moja tu baada ya Royal Armed Forces ,mabingwa wa zamani wa kombe hili kama Hearts of Oak kutimuliwa nje kwa pigo la mabao 3:0 huko visiwani Cape Verde.Duru ya kwanza wanajeshi hao wa Morocco wakiongoza kwa mabao 3,lakini Sporting Praia iliweza kusawazisha ,halafu chipukizi hao wa visiwa vya cape Verde wakawatimua wamorocco kupitia mikwaju ya penalty ya mabao 5-4.

Enyimba ya Nigeria yenye miadi duru ijayo na simba ya Tanzania na mwenzake Zamalek ya Misri ni mabingwa 2 wa zamani walioweza kutamba katika duru hii ya kwanza ya kombe hili.

Zamalek ikicheza bila ya mshambulizi wao hatari alieumia Amr Zaki ,iliwatandika APRC FC ya Rwanda mabao 2:0 mjini Cairo na kufuatilizia ushindi wake wa Kigali wa mabao 2:1.

Enyimba ya Nigeria ilitamba kwa mabao 3-2 mbele ya Diables Noires ya Kongo-Brazzaville.

Duru ijayo basi itazikutanisha Enyimba ya Nigeria na Simba ya Tanzania.TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo itakutana na wanajeshi wa Gabon FC 105 ya libreville.Mabingwa Al ahli ya Misri wana miadi duru ijayo na Al Tahrir ya eriotrea.Mamelodi Sundown ilioiadhibu Miembeni ya zanzibar itakutana na Curepipe Starlight ya Mauritius.Al Hilal ya Sudan itacheza na ZESCO United ya Zambia.

Kenya imerejea katika hali ya utulivu baada ya muwafaka uliofikiwa wiki iliopita.Je, kwa kadiri gani hii imefufua viwanja vya michezo nchini Kenya ?

Eric Ponda anasimulia:

Tukigeukia sasa Ligi mashuhuri za ulaya,Bayern Munich ilitamba jumamosi mbele ya mahasimu wao wakubwa Schalke 04 nyumbani mwa schalke-Gelsenkirchen ilipoondoka na bao 1:0 la Miroslav Klose.Hii ni mara ya kwanza kwa Bayern Munich kuondoka na ushindi katika uwanja wa schalke.Klose aliusindikiza mpira wavuni kutoka pasi ya mfaransa Franck Ribery.Wakisimulia maoni yao baada ya mpambano huo ambao waonesha haukuongoza kutimuliwa kwa kocha wa Schalke Marko Slomka aliesema:

„Ilikua shida kupata nafasi za kutia mabao.Nadhani lakini kwa jinsi mchezo wa utulivu na wa werevu kabisa ulioneshwa na Bayern munich ,ushindi wao ulistahiki.“

Nae kocha wa washindi na viongozi wa Ligi-Bayern Munich, Ottmar Hitzfeld alieleza:

„Mwishoe, tulipata bahati kwamba Schalke haikusawazisha.Kwani nadhani Schalke leo ingelistahiki kutoka nasi sare.“

Mahasimu wao wa karibu sana Werder Bremen walitamba nao nyumbani walipoikomoa Borussia Dortmund kwa mabao 2:0.Bochum iliistusha jana Bayer Leverkusen pale chipukizi hao walipoizima Leverkusen kwa mabao 2:0 na kuondoka na pointi 3.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza ,Arsenal London na Manchester United sasa zinapishana kwa pointi 1 tu kileleni.Manchester iliilaza Fulham kwa mabao 3:0 lakini Arsenal ilitoka sare 0:0 nyumbani Emirates Stadium kati yake na Aston Villa.

Arsenal sasa ina pointi 65 kutoka mapambano 28 wakati Manchester united ina pointi 64.Chelsea inanyatia nafasi ya 3 baada ya kluizima West ham kwa mabao4:0.

Real Madrid imerudisha mwanya wake wa pointi 5 kati yake na FC Barcelona katika La Liga –Ligi ya Spian kufuatia ushindi wao wa mabao 3-2 dhidi ya Recreativo Huelva.Barcelöona ililazwa mabao 4-2 na Atletico Madrid.

Katika serie A, viongozi wa Ligi Inter Milan walipata pigo lao la kwanza katika Ligi ya Itali msimu huu kutoka kwa Napoli.Marcelo Zalayeta alim,uadhibu kipa wa Brazil Julio Cesar kwa madhambi yake aliofanya dakika ya 3 ya mchezo.Sasa Inter Milan iko pointi 6 mbele ya AS Roma waliowapelekea salamu Real Madrid mahasimu wao jumatano hii ijayo katika champions League kwa kuizaba parma mabao 4-0.

Na huko Ufaransa, Olympique Lyon ilijiandaa kwa changamoto za wiki hii za chamnpions League kati yake na Manchester United kwa kuikomea Lille bao 1:0.