1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatma ya jimbo la Kosovo bado yajadiliwa

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRb

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wameapa kuwasilisha msimamo wa pamoja juu ya suala la uhuru wa jimbo la Kosovo hata kama mazungumzo kati ya Belgrade na Pristina yakivunjika.

Akizungumza baada ya kikao kischo rasmi mjini Viana Do Castelo nchini Ureno waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Lusi Amado alisema kuzuia mgawanyiko ni suala muhimu katika kuimarisha uaminifu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya.

Umoja huo umegawika juu ya ikiwa ulitambue jimbo la Kosovo indapo litajitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia au la.

Maafisa wa Serbia na Kosovo mwezi uliopita walianza mazungumzo ya mwisho ya kulitatua suala hilo la hatma ya jimbo la Kosovo mazungumzo hayo yanatarajiwa kukamilika Desemba 10. Serbia imesema haiwezi kukubali uhuru wa jimbo hilo na zimetishia pamoja na mshirika wake Urussi kutumia kura ya Veto dhidi ya mpango huo katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa