HAMBURG: Kansela Merkel asifu juhudi za kulinda mazingira | Habari za Ulimwengu | DW | 07.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAMBURG: Kansela Merkel asifu juhudi za kulinda mazingira

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema,Umoja wa Ulaya una dhima ya kuongoza katika juhudi za kulinda mazingira duniani.Katika mahojiano yake ametoa sifa kwa nchi za Umoja wa Ulaya na halmashauri ya umoja huo,ambazo zipo tayari kuchukua hatua za kupunguza gesi ya kaboni dayoksaidi inayochafua mazingira.Siku ya Alkhamisi,suala la kuhifadhi mazingira linatazamiwa kuwa mada kuu katika mkutano wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com