GAZA.Waziri mkuu atoa mwito wa kurejeshewa misaada ya kifedha
13 Februari 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniya ametowa mwito kwa Marekani na wapatanishi wengine katika mzozo wa mashariki ya kati wafunguwe misaada ya kifedha kwa serikali ya Palestina kufuatia mapatano mapya kati ya vyama vya Hamas na Fatah ya kuunda serikali ya umoja katika eneo hilo.