GAZA: Mapigano yaendelea kati ya Hamas na Fatah katika Ukanda wa Gaza. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Mapigano yaendelea kati ya Hamas na Fatah katika Ukanda wa Gaza.

Mapambano yangali yakiendelea kati ya makundi hasimu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Mapambano hayo yamekuwa yakiendelea ingawa vyama hivyo, Fatah na Hamas, vilikubaliana siku ya Ijumaa kukomesha uhasama.

Afisa wa usalama wa Fatah alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao makuu ya chama hicho.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah, na kiongozi wa Hamas, Khaled Meshall wamekubali kukutana mjini Makkah, Saudi Arabia siku ya Jumanne kujaribu kusuluhisha mzozo huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com