GAZA CITY: Wafuasi wa Fatah na Hamas wapambana upya | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY: Wafuasi wa Fatah na Hamas wapambana upya

Mapigano mapya yamezuka kati ya makundi hasimu ya Wapalestina,Hamas na Fatah katika mji wa Gaza.Mapambano hayo yametokea siku moja baada ya si chini ya Wapalestina 15 kuuawa na wengine darzeni kadhaa kujeruhiwa katika mapigano makali kabisa yaliozuka majuma ya hivi karibuni,kati ya makundi hayo.Kwa sababu ya machafuko hayo, majadiliano kuahirishwa kati ya Fatah na serikali inayoongozwa na Hamas.Tangu mapigano yalipoanza Alkhamisi usiku,wanachama 19 wa Hamas wametekwa nyara na wafuasi wa Fatah waliokuwa na silaha. Wakati huo huo wanachama 5 wa Fatah pia walitekwa nyara na wafuasi wa Hamas.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com