Freetown. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Freetown. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea.

Kazi ya kuhesabu kura inaendelea nchini Sierra Leone katika uchaguzi wake wa kwanza tangu majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda amani kuondoka nchini humo miaka miwili iliyopita.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa huenda ikahitajika duru ya pili ya uchaguzi kuweza kumpata rais mpya.

Wapiga kura walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya uchaguzi huo siku ya Jumamosi, ulioonekana kama mtihani wa uthabiti katika nchi hiyo ya Afrika magharibi baada ya miaka 11 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo Christiana Thorpe amesema kuwa uchaguzi huo wa rais na wabunge umekuwa wa kuaminika na wenye uwazi. Matokeo ya kwanza rasmi yanatarajiwa baadaye leo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com