FREETOWN: Viongozi wa zamani wa waasi kufungwa jela Sierra Leone | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FREETOWN: Viongozi wa zamani wa waasi kufungwa jela Sierra Leone

Mahakama maalum ya uhalifu nchini Sierra Leone,imetoa adhabu ya kufungwa jela muda mrefu,kwa viongozi wa zamani wa makundi ya waasi. Adhabu hiyo ni ya kufungwa jela kati ya miaka 45 na miaka 50.Jaji Julia Sebutinde aliesimamia kesi,alitangaza adhabu hiyo dhidi ya viongozi hao 3 wa zamani wa Majeshi ya Baraza la Kimapinduzi-AFRC.Kundi hilo katika mwaka 1997 lilimpindua rais aliechaguliwa, Ahmad Tejan Kabbah.Mwaka mmoja baadae,alirejeshwa madarakani kwa msaada wa vikosi vilivyoongozwa na Nigeria.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com