1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT:Benki kuu ya Ulaya yasaidia mabenki

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaN

Benki kuu ya Ulaya imesaidia mabenki ya hapa Ujerumani na euro bilioni 61 baada ya soko la mikopo kuyumbayumba kwasababu ya matatizo katika soko la uwekezaji la Marekani.Hatua hiyo haijapokelewa vizuri na masoko ya hisa kote ulimwenguni.Benki kuu ya Ulaya ECB inachukua hatua hiyo baada ya Benki kuu ya Japan kutia uero bilioni 6.12 katika masoko ya biashara nayo Marekani kuongeza dola bilioni 24 hapo jana.Hii ni mara ya kwanza kwa mabenki kuu ya Marekani,Ulaya na Japan kuchukua hatua ya pamoja tangu shambulizi la kigaidi kutokea mwezi Septemba mwaka 2001 nchini Marekani.Benki kuu za Australia,Hongkong na Canada aidha zimejiunga na hatua hiyo.Masoko ya hisa kote ulimwenguni yameyumba yumba hii leo huku FTSE ya London ikishuka kwa asilimia 2.9 CAC ya Paris kwa asilimia 2.4 na sarafu ya DAX ya Ujerumani kuporomoka kwa asilimia 1.8.Mgogoro huo unaleta wasiwasi juu ya kusababisha ugumu katika kupatikana mikopo kwa wawekezaji,vitega uchumi na makampuni.