1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

EU watasisitiza kuendelea kuisaidia Ukraine

Saumu Mwasimba
30 Januari 2024

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kusisitiza juu ya mwelekeo wao wa kuendelea kuisaidia Ukraine katika mkutano wa kilele utafaofanyika wiki hii mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/4bqgr
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borell Picha: Anwar Amro/AFP

Baraza la Ulaya tayari limeshasema kwamba kuna haja ya dharura ya kuongeza msaada wa silaha kwa Ukraine. Mkutano wa Brussels unasubiriwa wakati vita bado  vikiendelea ndani ya  Ukraine.

Urusi bado inaendelea kufyatuwa makombora yake kuelekea nchini Ukraine na hivi leo Jeshi la anga la Ukraine limearifu kwamba droni 35 za Urusi  zimeshambulia katika ardhi ya Ukraine, majira ya asubuhi na jumla ya droni 21 za Ukraine zilidunguliwa kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Urusi.

Soma pia:Urusi na Ukraine zashutumiana mashambulizi ya droni

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo ya ulinzi ya Urusi imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga  imezuia mashambulizi kadhaa ya droni za ukraine katika rasi ya Crimea na kwenye maeneo mengine manne usiku wa kuamkia leo.

Maeneo yaliyolengwa kwenye mashambulio hayo ni pamoja na mikoa ya Belgorod karibu na mpaka wa Ukraine, Bryansk,upande wa Magharibi na majimbo ya Kaluga na Tula Kusini mwa mji mkuu wa Urusi, Moscow. Hata hivyo taarifa hizo za Urusi hazikuweza kuthibitishwa na chombo huru. 

Mashambulizi ya Urusi usiku kucha dhidi ya Ukraine

Ripoti pia zilieleza kwamba wanajeshi wa Urusi walifyetuwa makombora aina ya S-300 ya kudunguwa ndege za kijeshi Mashariki wa Donetsk.

Ukraine | Mashambulizi ya Urusi
Mashambulizi ya droni za Urusi katika mikoa ya UkrainePicha: New Docs

Wakati vita vya Urusi vikiwa vinaonekana kuchachamaa upya nchini Ukraine viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kushinikiza hatua za kuendelea kuiongezea msaada wa kijeshi nchi hiyo wiki hii katika mkutano wao wa kilele utakaofanyika mjini Brussels,Ubelgiji. 

Soma pia:Blinken, Stoltenberg waonya mafanikio ya Ukraine

Katika waraka uliokwisha onekana na shirika la habari la Reuters kuelekea mkutano huo,ikilezwa kwamba baraza la Ulaya linasisitiza juu ya  haja ya dharura ya kupelekwa risasi na makombora nchini Ukraine.

Waraka huo pia haukutowa mwelekeo kuhusu suala la ikiwa viongozi watatoa ahadi ya kuchangia yuro bilioni 5 nyingine, kwenye kile kinachoitwa mfuko wa amani wa Ulaya,ambao kimsingi umekuwa ukitumika kukusanya michango ya kuinunua silaha Ukraine. Ukraine fedha zaidi kiasi yuro bilioni 5 za msaada.

Mvutano katika kutoa msaada zaidi kwa Ukraine

Kwa miezi sasa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekuwa wakivutana kuhusu mustakabali wa dhima ya mfuko huo wa fedha za kuisadia Ukraine kijeshi huku Ujerumani ikipendekeza kwamba mwelekeo hivi sasa uwe wa kutazama mchango unaotolewa na nchi moja moja.
 
Kwa upande mwingine Hungary ambayo mara zote ikizuia mipango ya kutowa msaada mkubwa kwa Ukraine inaelezwa kubadili msimamo.

Brussels, Ubelgiji |  Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa ba baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa ba baadhi ya viongozi wa Umoja wa UlayaPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Waziri mkuu Viktor Orban ameshathibitishayuko tayari kulegeza msimamo kuelekea mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuisaidia kifedha Ukraine kupitia mfuko wa bajeti ya Umoja huo. 

Sambamba na hayo Umoja wa Ulaya wenyewe umefikia makubaliano kuhusu hatua ya kwanza ya kuelekea matumizi ya mali za Urusi zinazoshikiliwa katika ukanda huo.

Soma pia:Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz azitolea mwito nchi wanachama wa EU waongeze msaada wa fedha kwa Ukraine

Umoja huo unataka kutumia faida itakayotokana na mali za Urusi zinazozuiwa kwenye taasisi za mataifa mbali mbali ya Ulaya,kuijenga upya Ukraine. 

Ikumbukwe kwamba mpaka sasa Umoja wa Ulaya unashikilia takriban yuro bilioni 200 za benki kuu ya Urusiambapo asilimia 90 ya fedha hizo zinashikiliwa na Taasisi ya fedha ya Kimataifa ya Euroclear yenye makao yake Ubelgiji.