1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aitolea mwito EU waongeze msaada wa fedha kwa Ukraine

Saumu Mwasimba
29 Januari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amezitolea mwito nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuongeza msaada kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4bmka
Berlin | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Ruffer/Caro/picture alliance

Akizungumza jana mbele ya mkutano wa chama chake cha Social Democratic SPD mjini Berlin, Scholz alisema serikali ya Ujerumani imetenga zaidi ya yuro bilioni 7 kwaajili ya Ukraine katika bajeti ya mwaka huu 2024, kiwango ambacho amesema ni zaidi ya nusu ya mchango uliotolewa na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.

"Ningependa sisi katika Umoja wa Ulaya tuzungumzie kuhusu namna kila mmoja anavyoweza kuongeza mchango wake. Haiwezekani kwamba Ujerumani ndiyo inayotowa mchango mkubwa.''

Hungary ambayo inapinga msaada zaidi wa kifedha kwa Ukraine, leo imeonesha kuwa tayari kuruhusu pendekezo la Umoja wa Ulaya la kuipatia msaada wa kifedha Ukraine kutoka kwenye bajeti ya Umoja huo.

Hatua ya Hungary imekuja wakati Umoja huo unapanga kukutana kwa mkutano wa dharura wa kilele Alhamisi wiki hii.