1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi na Ukraine zashutumiana mashambulizi ya droni

30 Januari 2024

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kikosi cha anga cha nchi hiyo kimesema kimezuia mashambulizi kadhaa ya droni katika eneo la rasi ya Crimea, huku Ukraine nayo ikiishutumu Urusi kufanya mashambulizi ya droni 35.

https://p.dw.com/p/4bpUi
Rasi ya Crimea | Daraja la Crimea baada ya kushambuliwa na Ukraine
Moshi ukifuka katika daraja la Crimea baada ya shambulizi la UkrainePicha: Alyona Popova/TASS/dpa/picture alliance

Wizara ya ulinzi Urusi katika taarifa yake imesema kwamba jumla ya droni ishirini na moja za Ukraine zilidunguliwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Crimea, Belgorod na miko ilio kusini mwa mji mkuu wa Moscow ya Kaluga na Tula ililengwa pia.

Moscow imesema kuwa droni kumi na moja za Ukraine kati ya ishirini na moja pekee zilidunguliwa skatika eneo la Bahari Nyeusi katika rasi ya Crimea, haliki hakujaripotiwa uharibifu wa aina yoyote hadi sasa.

Hata hivyo taarifa hizo hazikuweza kuthibitishwa katika uwanja wa vita.

Soma pia:Blinken, Stoltenberg waonya mafanikio ya Ukraine

Katika kile kinachotajwa kuendeleza makabiliano katika ya vikosi vya Urusi na Ukraine, Kyiv imesema imedungua droni takriban 15 kati ya 35 katika mikoa ya Mykolaiv, Sumy, Kharkiv na maeneo mengine ya kimkakati.

Urusi ambayo imekuwa ikiendesha vita vya kila upande dhidi ya Ukraine kwa takriban miaka miwili sasa, imekuwa ikishambulia nchi hiyo jirani mara kwa mara kwa droni na makombora.

Watu wawili wameuwawa, wengine wamejeruhiwa

Ukraine imesema leo kwamba watu wawili wameuawa na takriban wengine watano kujeruhiwa katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo ya Urusi yaliyolenga miundombinu ya kijeshi na nishati.

Sloviansk, Ukraine | Mkaazi akiangalia mabaki ya jengo la makaazi
Mkaazi akitazama jengo la makaazi baada ya kushambuliwa na droni za Urusi katika mashambulizi ya usiku kucha.Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Kyiv alisema vikosi vya Urusi vimerusha makombora mawili na droni 35 kote Ukraine na  20 kati ya droni hizo zenye chapa (UAVs) zilikwepa mifumo ya ulinzi wa anga.

Jeshi la anga la Ukraine katika taarifa yake kwa umma iliongeza kuwa, droni za Urusi zilizolenga kushambulia maeneo ya kimkakati, zilijaribu kupiga miundombinu ya mafuta na nishati, na miundombinu ya kiraia na kijeshi.

Vikosi vya Urusi pia vimevurumisha makombora mawili chapa S-300 ya kudungulia makombora na kushambulia mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk.

Soma pia:Mahakama ya ICJ kutoa uamuzi ikiwa inayo mamlaka ya kusikiliza kesi iliyofikishwa na Ukraine dhidi ya Urusi

Kulingana na mamlaka katika maeneo husika moto mkubwa ulizunga katika eneo la Dnipropetrovsk baada ya mashambulizi ya droni ya Urusi na kuuwa watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa.

"Mwanamume mwenye umri wa miaka 38 ambaye alikuwa akiendesha baiskeli aliuawa kutokana na shambulio.Waendesha mashtaka katika eneo hilo walisema katika taarifa yao.

Waliongeza kuwa  mwanamke mwenye umri wa miaka 50 alijeruhiwa na alipelekwa hospitali,kwa ajili ya matibabu ya haraka.

kyiv ambayo imekuwa ikipokea msaada wa zana za kivita kutoka kwa washirika wake wa magharibi ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga, imekuwa ikijibu mashambulizi.

Ujerumani: Hatutaiacha Ukraine kwenye vita peke yake

Crimea, ambayo iliunganishwa na Urusi mwaka 2014 kwa kukiuka sheria ya kimataifa, imekuwa lengo la mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukraine, tangu Moscow ilipofanya uvamizi kamili kwa jirani yake mnamo Februari 24, 2022.

EU: Bado tutaendelea kuiunga mkono Ukraine

Kulingana na rasimu ya hitimisho la mkutano wa kilele siku wa siku ya Alhamisi, viongozi wa Umoja wa Ulayawatasisitiza azma yao ya kutoa "msaada wa kijeshi kwa wakati unaofaa, unaotabirika na endelevu" kwa Ukraine.

Soma pia:Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz azitolea mwito nchi wanachama wa EU waongeze msaada wa fedha kwa Ukraine

Sehemu ya rasimu hiyo ya maandishi imesisitiza kuwa "baraza la Ulaya pia linasisitiza hitaji la dharura la kuharakisha utoaji wa risasi na makombora," kwa Kyiv.