1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Putin ailaumu Ukraine kuhusu ajali ya ndege

Tatu Karema
27 Januari 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameahidi kuweka hadharani matokeo ya uchunguzi wa nchi yake kuhusu ajali ya ndege ambayo anadai kuwa vikosi vya Ukraine viliidungua

https://p.dw.com/p/4bjmL
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa mkutano wa kila  mwaka na waandishi wa habari mjini Moscow mnamo Desemba 14,2023
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Katika matamshi yake ya kwanza hadharani kuhusu ajali hiyo ya Jumatano, Putin alirudia matamshi yaliotolewa awali na maafisa wa Urusi kwamba "kila kitu kilipangwa" kwa kubadilishana wafungwa siku hiyo wakati ndege ya kijeshi chapa IL-76 ilipoanguka katika eneo la mashambani la mkoa wa Belgorod nchini Urusi ikiwa imewabeba wafungwa wa kivita 65 wa Ukraine.

Soma pia:Urusi inadai ndege iliyodunguliwa ilikuwa na wanajeshi wa Ukraine

Putin hakutoa maelezo yoyote kuunga mkono madai hayo kwamba Ukraine ndiyo ya kulaumiwa.

Maafisa wa Ukraine pia hawajasema iwapo jeshi lake liliidungua ndege hiyo, lakini wametoa wito wa uchunguzi wa kimataifa.