1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

EU yaishutumu Belarus kwa ukandamizaji

Tatu Karema
26 Januari 2024

EU na Marekani zimeishtumu Belarus kwa kufanya mfululizo wa mashambulizi ya kisiasa wiki hii, huku mashirika ya haki yakisema zaidi ya watu 150 walizuiliwa au kuhojiwa na idara ya usalama KGB ndani ya siku moja

https://p.dw.com/p/4bguM
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Minsk, Alhamisi Julai 6, 2023
Rais wa Belarus Alexander LukashenkoPicha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel, amesema Umoja huo unashtumu vikali wimbi la ukandamizaji la hivi karibuni dhidi ya wafungwa wa zamani wa kisiasa waliosalia Belarus pamoja na jamaa za wafungwa hao.

Marekani yaahidi hatua zaidi dhidi ya Belarus

Marekani pia imeshtumu mashambulizi hayo makubwa yanayofanywa na utawala wa Belarus dhidi ya haki za binadamu na majaribio ya kuzima matarajio ya kidemokrasia ya watu wa Belarus.

Soma pia:Putin na Lukashenko wafanya mazungumzo Urusi

Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, amesema wataendelea kuuwajibisha utawala wa Belarus kupitia vikwazo na njia nyinginezo, kwa ukandamizaji wake mkali wa ndani pamoja na uungaji wake mkono wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.