1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliouawa kwa makombora ya Urusi wafikia 11

26 Januari 2024

Maafisa wa Ukraine wamesema idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya makombora ya Urusi kwenye mji wa Kharkiv imeongezeka na kufikia watu 11.

https://p.dw.com/p/4bhaz
Ukraine | Urusi | Kharkiv
Madhara ya mashambulizi ya Urusi katika mji wa Kharkiv.Picha: Ukrainian Emergency Service/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Kharkiv imeeleza kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 61 ameuawa leo kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata, na kuongeza idadi ya waliofariki katika mji huo kuwa watu 11.

Katika moja ya mashambulizi makubwa ya angani, zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa na wengine 18 waliuawa baada ya makombora ya Urusi kulenga mji mkuu, Kiev, na mji wa kaskazini mashariki mwa Kharkiv mapema siku ya Jumatatu (Januari 22).

Soma zaidi: Ndege ya kijeshi ya Urusi yaanguka na kuua watu wote 74

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kujibu kwa nguvu mashambulizi hayo ya Urusi.

Katika tukio tofauti, mamlaka ya Ukraine katika eneo la Donetsk ambayo sehemu yake iko chini ya udhibiti wa Urusi, imesema watu sita wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Urusi jana Alhamisi.