Dortmund mabingwa wa Bundesliga 2011 | Michezo | DW | 30.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Dortmund mabingwa wa Bundesliga 2011

Borussia Dortmund leo wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa soka nchini Ujerumani baada ya kuifunga Nuremberg mabao 2-0, huku Bayern Leverkuessen ikichapwa mabao 2-0 na FC Cologne.

default

Matokeo hayo yameifanya Dortmund kufikisha pointi 72 ambazo haiwezi kufikiwa na timu yoyote ile katika michezo miwili iliyosalia kuhitimisha Bundesliga.

Mara ya mwisho kwa Dortmund kutwaa ubingwa wa Bundesliga ilikuwa mwaka. 2002 na ni mara ya saba kwa timu hiyo kutwaa uchampion huo.Leverkusen, anaendelea kubakia katika nafasi ya pili.

Mwandishi: Aboubakary Liongo/Reuters/DPA

Mhariri: Mohamed Dahman

DW inapendekeza