DHAKA: Gavana wa zamani wa benki kuu ateuliwa kuongoza serikali ya mpito
12 Januari 2007Matangazo
Rais Iajuddin Ahmed wa Bangladesh amemteua gavana a zamani wa benki kuu ya nchi hiyo, Fakhruddin Ahmed kuiongoza serikali ya mpito. Fakhruddin ana jukumu la kuandaa uchaguzi mkuu nchi humo baada ya rais Iajuddin Ahmed kuuahirisha alipojiuzulu wadhifa wake.
Akilihutubia taifa kwenye runinga, rais Ahmed alitangaza pia hali ya tahadhari nchini Bangladesh.
Uchaguzi mkuu ulikuwa umepangwa ufanyike tarehe 22 mwezi huu. Kufikia sasa tarehe ya uchaguzi bado haijatangazwa.