CAIRO: Uamuzi wa Marekani kutumia kura ya turufu umekosolewa | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO: Uamuzi wa Marekani kutumia kura ya turufu umekosolewa

Umoja wa nchi za Kiarabu umekosoa kura ya turufu iliyopigwa na Marekani katika Baraza la Usalama kuhusika na mswada wa azimio uliotoa mwito wa kuilaumu Israel kwa shambulio lake la hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza.Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu,Amr Mussa alipozungumza kabla ya kikao cha dharura cha umoja huo mjini Cairo,alisema uamuzi wa Marekani umepokea kwa huzuni na hamaki.Kura ya turufu ni hatua isiyoeleweka na humaanisha kuwa utaratibu wa amani umekwisha.Akiendelea alisema Israel itaitumia kura ya turufu ya Marekani kama kisingizio cha kuendelea na mashambulio yake dhidi ya Wapalestina.Kufuatia pendekezo la Lebanon,umoja huo mjini Cairo utaijadili hali ya hivi sasa ya maeneo ya Wapalestina na hasa kuhusu shambulio la siku ya Jumatano katika mji wa Beit Hanoun.Shambulio hilo la Israel lilisababisha vifo vya Wapalestina 18.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com