Bunge la Libanon limeahirisha kumchagua rais mpya
23 Novemba 2007Matangazo
Bunge la Libanon limeahirisha kumchagua rais mpya hadi Novemba 30,nchi hiyo ikakabiliwa na mgogoro wa kisiasa.Chama kinachoelemea kambi ya Magharibi na kile kinachoiunga mkono Syria,vimeshindwa kuafikiana nani atakaechukua nafasi ya Rais wa sasa Emile Lahoud,ambae awamu yake inamalizika leo usiku wa manane.