BERLIN:Wafanyikazi wa Deutsche bahn i kutogoma mpaka baada ya mazungumzo | Habari za Ulimwengu | DW | 10.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Wafanyikazi wa Deutsche bahn i kutogoma mpaka baada ya mazungumzo

Shirika la Wafanyikazi wa reli linatangaza kuwa halitafanya migomo zaidi mpaka baada ya awamu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu suala la malipo kufanyika.Mazungumzo hayo yanawaleta pamoja wawakilishi wa shirika hilo na kampuni ya treni ya kitaifa ya Deutsche Bahn.Hatua hii inatokea baada ya madereva wa treni katika miji ya Hamburg na Berlin kusitisha huduma zao kwa saa mbili wakati wa asubuhi ulio na wasafiri wengi.Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya asilimia 31 ya mshahara huku kampuni ya Deutsche Bahn ikikubali kutoa asilimia 4 u nusu pekee.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com