BERLIN:Tume ya Ulaya yatoa sera mpya ya nishati
10 Januari 2007Matangazo
Tume ya Ulaya inapanga kutoa mkakati mpya wa nishati kwa Ulaya hii leo.Ripoti hiyo inaazimia kulenga athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa kupigia debe utumiaji wa nishati ya nuklia vilevile kuimarisha viwango vya vichochezi vinavyoweza kutumia tena na tena.Aidha inatarajiwa kupunguza hali ya kutegemea nishati kutoka mataifa ya kigeni ya mafuta na gesi barani Ulaya.Kulinga na Umoja wa Ulaya matumizi ya nishati yanapaswa kubadilika la sivyo ifikapo mwaka 2030 asilimia 65 ya nishati ya Ulaya italazimika kununuliwa kutoka mataifa ya kigeni.Uamuzi wa mapendekezo hayo unatarajiwa mwezi machi.