Berlin. Wajerumani washutumu siasa kali za mrengo wa kulia katika maandamano. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Wajerumani washutumu siasa kali za mrengo wa kulia katika maandamano.

Katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin mamia ya watu wamefanya maandamano ya amani kupinga dhidi ya mkutano mjini humo wa chama chenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, cha NPD.

Kiasi watu wanaokadiriwa kufikia 400 waliandamana wakiwazomea wajumbe 500 wa chama cha NPD ambao wamejikusanya kwa ajili ya mkutano wa chama chao.

Chama cha NPD kina viti vichache katika mabaraza mawili ya majimbo katika eneo la mashariki ya Ujerumani lakini hakina viti katika bunge la shirikisho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com