BERLIN : Wafanyakazi wa reli kufanya migomo ya onyo | Habari za Ulimwengu | DW | 01.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Wafanyakazi wa reli kufanya migomo ya onyo

Wafanyakazi wa reli wa Ujerumani wataanza migomo ya omyo hapo kesho baada ya mazungumzo ya kudai nyongeza ya mishahara kati ya vyama vya wafanyakazi na shirika la reli linalomilikiwa na taifa Deutsche Bahn kusambaratika.

Naibu mkuu wa chama cha Transnet Regina Rusch-Ziemba amesema mgomo wa kwanza utaanza wakati wa usiku katika mji wa magharibi wa Dortmund ukifuatiwa na migomo mengine ya onyo mapema asubuhi.

Migomo zaidi itaendelea nchini kote Ujerumani katika kipindi cha wiki na inatazamiwa kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria.

Shirika kuu la reli nchini la Deutsche Bahn limekataa madai ya vyama vya wafanyakazi kupandisha mishahara ya wafanyakazi 134,000 kwa asilimia saba.Badala yake imekubali kupandisha mishahara hiyo kwa asilimia mbili tu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com