BERLIN: Mwito wa kutuma vikosi kulinda amani jimbo la Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 26.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Mwito wa kutuma vikosi kulinda amani jimbo la Darfur

Waziri wa ushirikiano wa uchumi na maendeleo wa Ujerumani,Heidemarie Wieczorek-Zeul ametoa mwito kwa jeshi la Ujerumani kupeleka vikosi vyake katika jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan, ikiwa Umoja wa Mataifa utaomba msaada wa Berlin.Katika mahojiano yake na gazeti la „Bild am Sonntag“,waziri huyo amesema Ujerumani haiwezi kukataa ombi kama hilo ikiwa Umoja wa Mataifa utahitaji msaada.Amesema,mauaji ya halaiki yanatokea pole pole.Hivi sasa wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika wapo Darfur,lakini wameshindwa kuzuia mapigano katika jimbo hilo la magharibi. Umoja wa Mataifa umependekeza kupokea ujumbe huo,lakini serikali ya Sudan inapinga.Mashirika yanayotoa misaada ya kiutu yanasema watu 200,000 wamefariki kwa sababu ya vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu.Kiasi ya watu milioni 3 pia wamelazimika kukimbia makwao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com