BERLIN : Mwenyekiti wa bodi ya Siemens kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Mwenyekiti wa bodi ya Siemens kujiuzulu

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vinaripoti kwamba mwenyekiti wa bodi ya Siemens kampuni kubwa kabisa ya Kijerumani Heinrich von Pierer atatangaza kujiuzulu kwake leo hii.

Gazeti mashuhuri la Bild limesema von Pierer ataachia wadhifa wake katika mkutano ujao wa bodi hapo tarehe 25 mwezi wa April.Von Pierer amesema anajiuzulu ili kuwajibika binafsi kwa uchunguzi wa rushwa wa kampuni hiyo yenye makao yake mjini Munich.

Waendesha mashtaka wanachunguza madai ya malipo yasio halali ya kujipatia biashara nchi za nje na wakuu watendaji wa hivi sasa na wa zamani wamehojiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo mwanachama wa bodi Gerhard Cromme atachukuwa nafasi ya von Pierer ambaye kipindi chake cha uongozi kilikuwa kimalizike mwakani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com