BERLIN : Muafaka kwa mageuzi ya huduma za afya | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Muafaka kwa mageuzi ya huduma za afya

Waziri mkuu wa Israel na rais George W. Bush

Waziri mkuu wa Israel na rais George W. Bush

Waziri wa Afya wa Ujerumani amesema umefikiwa muafaka wa mwisho juu ya mipango ya kuufanyia mageuzi mfumo wa huduma za afya nchini wa euro bilioni 140.

Waziri wa Afya Ulla Schmidt ameulezea muafaka huo uliofikiwa na vyama mbali mbali kuwa ni ushindi.Amesema rasimu ya sheria hiyo iliofanyiwa marekebisho itaweza kufikishwa bungeni ili kuidhinishwa hivi karibuni ina inatazamiwa kuanza kazi tarehe Mosi mwezi wa April.

Mpango huo wa mageuzi ya huduma za afya unakusudia kupunguza gharama kubwa za mfumo wa huduma za afya nchini Ujerumani na kuufanya uwe wa wazi kwa wafanyakazi wanaougharimia kwa kupitia michango ya lazima.

Wanaoukosowa mpango huo mpya wanasema mabadiliko hayo hayotosaidia sana kutatuwa tatizo la muda mrefu la kuwaondolea mzigo wa michango wafanyakazi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com