BERLIN: Mfungwa wa zamani wa Guantanamo, Murat Kunaz aeleza hali ya Marekani kukiuka haki za binadamu nchini Afghanistan. | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Mfungwa wa zamani wa Guantanamo, Murat Kunaz aeleza hali ya Marekani kukiuka haki za binadamu nchini Afghanistan.

Mfungwa wa zamani wa gereza la Guantanamo, Murat Kurnaz ameieleza tume ya uchunguzi ya bunge la Ujerumani kuhusu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyofanywa katika kambi Marekani nchini Afghanistan.

Murat Kurnaz, mturuki ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani aliwaambia wabunge kwamba alikuwa akifungwa kwa minyororo na kuning`inizwa kwa siku kadhaa hadi madaktari walipokuja kumchunguza iwapo mwili wake ungestahamili mateso hayo.

Murat Kurnaz aliyarejea madai yake kwamba askari wawili wa Kijerumani walimpiga wakati akizuiliwa nchini Afghanistan.

Kurnaz alikamatwa mwaka 2002 nchini Pakistan na kupelekwa Guantanamo Bay kisha akaachiwa huru bila kushtakiwa mwaka uliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com