BERLIN: Merkel apinga uanachama wa China katika mataifa ya G8 | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Merkel apinga uanachama wa China katika mataifa ya G8

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, amepinga uanachama wa China katika mataifa yaliyoendelea kiviwanda ya G8.

Akizungumza katika kikao cha leo cha baraza lake la mawaziri mjini Berlin, Bi Merkel amesema hana mpango wowote wa kujadili swala hilo atakapochukua urais wa mataifa ya G8 mwaka ujao.

Afisa wa ngazi ya juu mjini Berlin, ambaye hakutana jina lake litajwe, amesema kuna sababu mbili kwa nini Ujerumani imechukua msimao huo. Kwanza, muungano wa mataifa ya G8 ni jamii ya maadili na pili, Ujerumani haitaki muungano huo upanuke na kuwa mkubwa.

Afisa huyo amekiri kwamba uchumi wa China umeshinda uchumi wa baadhi ya mataifa wanachama wa G8, lakini hata hivyo akasema kansela Angela Merkel anafikri wakati haujafika wa kuiruhusu China iwe mwanachama wa G8.

Mkutano wa baraza la mawaziri umezungumzia juu ya malengo ya Ujerumani itakapochukua uongozi wa G8 mwaka ujao, masoko ya uuzaji wa mafuta, mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo barani Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com