1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki Kuu duniani zachukua hatua za dharura kuunusuru uchumi

jk9 Oktoba 2008

Benki Kuu karibu kote duniani zimechukua hatua za dharura kudhibiti mzozo unayoyakabili masoko fedha.

https://p.dw.com/p/FWdD
Madalali wakiwa wameduwaa kutokana na kuporomoka kwa hisa katika soko la hisa la Ujerumani mjini FrankfurtPicha: AP

Katika hatua hizo, Benki Kuu za Ulaya,Marekani, Uingereza na nyinginezo ikiwemo ya China zimepunguza viwango vya riba, katika kukabiliana na hali hiyo.


Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa ambaye nchi yake kwa sasa ndiyo inayoshikilia kiti cha urais wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kunyanyua uchumi wa dunia na kwamba umoja huo kwa sasa unajadili hatua zaidi za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.


Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa tatizo hilo ambalo limeikumba dunia nzima linahitaji ushirikiano wa nchi zote kuweza kupata ufumbuzi.


Mjini Washington Rais George Bush wa Marekani amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kujadiliana jinsi ya kukabiliana na mzozo huo wa fedha duniani.Rais Bush pia alizungumza na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil.


Nalo Shirika la Fedha duniani IMF limeonya ya kwamba mzozo huo wakiuchumi duniani umeingia katika hatua ya mbaya kuwahi kutikisa masoko ya fedha toka miaka ya 1930.


Katika ripoti yake ya tathimini ya uchumi duniani, shirika hilo limesema kuwa kutokana na mzozo huo uchumi wa dunia utakuwa kwa polepole mwakani, na kutabiri kuwa uchumi wa Ujerumani hautokuwa kama ilivyokuwa mwaka huu.Mwaka huu uchumi wa Ujerumani ulikuwa kwa asilimia 1.8