BEIJING: Rais wa Ufaransa Jacques Chirac ziarani China
25 Oktoba 2006Matangazo
Rais wa Ufaransa, Jaques Chirac, amewasili leo mjini Beijing China kwa ziara rasmi ya siku nne inayotarajiwa kuboresha mahusiano kati ya China na Ufaransa.
Rais Chirac anatarajiwa kuzungumzia mzozo wa nyuklia wa Korea Kaskazini na kuitaka China ilishughulikie swala la haki za binadamu.
Rais Chirac ameandamana na viongozi 30 wa viwanda na wanataraji kusaini mikataba ya kibiashara ikiwa ni pamoja na mkataba wa kampuni ya Airbus na kampuni ya Alstom kuiuzia China treni 500.