1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama laidhinisha muongozo kuhusu amani Libya

Sekione Kitojo
13 Februari 2020

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha vifungu 55 vya muongozo utakaomaliza vita nchini Libya na kushutumu ongezeko  la matumizi ya nguvu katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ya Afrika ya kaskazini. 

https://p.dw.com/p/3XhO2
UN-Sicherheitsrat 2011
Picha: AP

Azimio lililoidhinishwa na baraza  la  Usalama pia  limetoa wito  wa  kuwapo  na usitishaji  wa  kudumu  wa  mapigano nchini  Libya, ambako makubaliano tete ya  kusitisha  mapigano yamekuwapo  tangu  Januari mwaka  huu. 

USA Sitzung des UN-Sicherheitsrats in New York - Vasily Nebenzya
Mwakilishi wa kudumu wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vasily NebenzyaPicha: Reuters/B. McDermid

Azimio hilo  lililotayarishwa  na  Uingereza , liliidhinishwa kwa  kura  14 kati  ya  15, ambapo  Urusi  imejizuwia kupiga  kura, licha  ya  kuwa  rais  wa  Urusi Vladimir Putin alikuwa  mmoja  wa  viongozi 12 waliokubaliana  na mpango  huo  katika  mkutano  mjini  Berlin  Januari 19. Balozi  wa  Urusi  katika  Umoja  wa  mataifa  Vassily Nebenzia  amesema  amejizuwia  kupiga  kura  kwasababu serikali  yake  ina wasiwasi  mkubwa , juu  ya  iwapo  azimio hilo linaweza  kutekelezwa  na  kumaliza  vita  kati  ya serikali  hasimu, katika  njia  ambayo  tungependa  kuiona.

"Tuna  wasi  wasi mkubwa iwapo  aina  hii  ya  kauli ya mwisho itawawezesha  Walibya  kufikia  makubaliano haraka. Kwa kweli  tungependa  maazimio  ya  baraza  la Usalama  kutekelezwa. Tungependa  azimio  hili lifanyekazi. Hata  hivyo  sidhani  kama  maelezo ya azimio hili yanawezekana.

Libyen Tripolis Kämpfer der GNA
Wapiganaji wa majeshi ya serikali inayoungwa mkono kimataifa mjini Tripoli wakijitayarisha kwa mapambanoPicha: picture-alliance/Photoshot/H. Turkia

"Matukio yataonesha  nani  yuko  sahihi," amesema Nebenzia. Na  iwapo  azimio  hilo litakuwa  na  athari chanya  katika  kutatua mzozo  huo, nitakuwa  wa  kwanza kukiri kwamba  nilikosea."

Azimio  hilo limesisitiza , "haja  ya  kuwapo  na  usitishaji wa  kudumu  ya  vita  nchini  Libya  haraka  iwezekanavyo, bila  ya  masharti  yoyote. Pia  azimio  hilo  limeeleza  wasi wasi  kuhusu ongezeko  la  kuhusika  kwa  wapiganaji mamluki  nchini Libya.

Naibu mwakilishi wa  kudumu wa Ujerumani  katika  Umoja wa  Mataifa  Juergen Schultz  amesema azimio  hilo linatuma  ujumbe  kwa  Libya.

Deutschland Libyen-Konferenz in Berlin
Wawakilishi maalum na mkuu wa ujumbe wa usaidizi nchini Libya Ghassan Salame (kushoto) pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres na kansela wa Ujerumani(katikati) katika mkutano wa Berlin kuhusu LibyaPicha: AFP/M. Kappeler

"Kwa  kuidhinishwa  azimio  hili, baraza  la  Usalama linatuma  ishara  muhimu  kwa  amani  nchini  Libya, likisisitiza  nia  sahihi  ya  washiriki wote wa  mkutano  wa Berlin. Ni  muhimu  kwa  Libya  kwamba  tumeweza kutuma  ishara  hii  ya  Umoja."

Balozi  wa  Uingereza  amepinga  kauli  ya  balozi  wa Urusi na  kusema  azimio  hilo linawezekana, akisema  kile inachokifanya , ni  kutoa maelezo sahihi  ya  nia  ambazo viongozi  waliidhinisha  mjini  Berlin, na  hii  ni  pamoja  na rais Putin wa  Urusi.