1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wanajeshi zaidi wa Marekani wauwawa.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZF

Majeshi ya Marekani nchini Iraq yameripoti watu zaidi waliouwawa kutokana na vifo vya wafanyakazi 21 wa jeshi hilo.

Kuanguka kwa helikopta ya jeshi la Marekani kaskazini mashariki ya mji wa Baghdad kumesababisha vifo vya wanajeshi 13 siku ya Jumamosi.

Jeshi hilo limesema sababu ya kuanguka kwa helikopta hiyo bado hakujajulikana .

Saa chache baadaye , jeshi la Marekani limesema wanajeshi wake watano wameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika mapigano na wanamgambo katika mji wa Washia wa Karbala upande wa kusini. Mwanajeshi mwingine ameuwawa katika bomu lililotegwa kando ya barabara mjini Baghdad.

Jeshi la Marekani pia limesema kuwa wanajeshi wengine wawili waliuwawa siku ya Ijumaa. Vifo hivyo vinakuja wakati vikosi vya kwanza vya wanajeshi karibu 21,000 vya nyongeza vimeanza kuwasili nchini Iraq katika mpango wa rais wa Bush wa kutuma wanajeshi zaidi nchini humo.