Baghdad. Wanajeshi wengine wa Marekani wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 22.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Wanajeshi wengine wa Marekani wauwawa.

Kiasi cha watu 15 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Suleiman Beg.

Mji huo uko kilometa 90 kusini mwa Kirkuk. Polisi wamesema kuwa mtu huyo aliyejitoa muhanga aliigonga gari yake katika jengo la halmashauri ya jiji kabla ya kujilipua.

Wakati huo huo , wanajeshi watano wa Marekani wameuwawa katika shambulio la bomu kando ya barabara kusini magharibi ya mji wa Baghdad. Vifo hivyo vimetokea wakati wanajeshi wa Marekani na wale wa Iraq wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji ndani na kuzunguka mji huo mkuu wa Iraq.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa kiasi cha wapiganaji 41 wameuwawa hadi sasa, na idadi kubwa ya silaha zimekamatwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com